DOLA LA ZANZIBAR

Tags

Dola la Zanzibar
Zanzibar ikiwa ni taifa kamili, lina haki kamili ya kuwa na vyama vyake huru vya kisiasa bila ya kulazimishwa kuungana na chama chochote cha Taifa la Tanganyika, ambalo vile vile ni taifa huru. Taifa, Dola au Nchi haziundwi kutokana na ndoto za mtu mmoja au watu wachache. Ili taifa litambulike kama taifa, kunahitajika sifa maalum za lazima na sio za kulazimishwa, kuzushwa au kubuniwa. Kwa mujib wa sifa za kimataifa Zanzibar ni nchi na taifa kamili – bila ya kujali nani ana au wanabuni vyengine. Nchi ye nye mipaka inayotambulika kimataifa, na kuwa na watu wenye sifa maalum za nchi hiyo, kwa kusema lugha inayotambulika kuwa lugha ya au za nchi hiyo, yenye utamaduni na kabila au makabila ya nchi hiyo, yenye jamii halisi na makhsusan, siasa inayoifuata na uchumi wake wa kujitegemea wenyewe, inatambulika kama ni nchi, aidha ikiwa huru au ikiwa imetawaliwa, yaani kama Zanzibar ilivyokuwa chini ya ukoloni wa Kiingereza (na hata ukoloni wa sasa). Nchi kama hiyo ikiwa huru inatambulika na Umoja wa Mataifa kama ni Nchi na Taifa huru. Bila ya haja ya kukariri zaidi Zanzibar inazo sifa zote ambazo zina hitajika ili nchi itam- bulike kama taifa huru, pamoja na kuwa na kiti chake katika Umoja wa Mataifa, ambacho kipo wazi tokea kuundwa Muungano katika mwaka 1964. Kabla ya kuruhusiwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa Tanzania, Zanzibar iliwekewa pingamizi na vikwazo vya kutounda vyama vyake huru, na ilihitajika na kulazimika kwamba vile vyama vitakavyoundwa viwe na sifa za "Kitaifa" na visiwevya kijimbo, kidini n.k. kama alivyobuni Julius K. Nyerere. Kwa vile nchi ilikuwa chini ya utawala wa chama kimoja chenye kawli na amri ya mwisho, Wazanzibari na Watanganyika ikawabidi, shingo upande wafuate kauli na amri ya watawala wao, wananchi wa nchi mbili hizo wakisubiri kwa hamu kubwa, siku mambo yatakavyobadilika, na hatimae kuyabadilisha masharti hayo. Wengi zaidi ya Wazanzibari na Watanganyika, ambao pia ni wenye sifa za kuwa nchi na taifa huru, hawakuamini kwamba Tanzania ni nchi au ni taifa, kama isemekanavyo. Tanzania ni nchi na taifa la kubuni, kama taifa la ndotoni na sio nchi au taifa halisi kwa mujib wa tafsiri za kimataifa zinavyotambulika.

Tanzania si nchi wala si dola, bali ni Muungano wa nchi/taifa mbili huru zote mbili zi- likuwa na uwakilishaji kamili katika Jumuiya ya Madola.Muungano wa Tanzania ni sawa na Muungano wa Misri na Syria,"United Arab Republic" ambao umeshavunjika kwa hivi sasa na kubaki jina tupu, na kila nchi kuwa na mamlaka yake wenyewe. Mfano mwengine ni Muungano au shirikisho la Kisovieti-ambalo limeshamungunyika na mfano mwengine ukiwa Muungano/shirikisho la iliyokuwa Yugoslavia;- tofauti na hali hiyo ni Vietnam am- bayo ni nchi mmoja na imeshaungana, wakati Korea ikiwa na serikali mbili katika nchi moja zilizotengwa na ukoloni kwa maslahi ya kikoloni. Muungano wa Tanzania ni sawa na muungano waUingereza na Irelandya kaskazini yaani baina ya mtawala na mtawaliwa, ingawa Ireland inaweza kuunda vyama vyenye sifa ya Kiireland tofauti na Zanzibar. Mtu au Chama tawala kinaweza kulazimisha watu wafuate na kuitii fikra au sheria fulani, lakini hawawezi kulazimisha watu kuamini fikra hiyo ya kubuni, kama vile mtu anaweza kula zimishwa kuamini kuwa nyoka ana miguu, lakini kutoweza kumfanya mtu huyo aamini hivyo. Mzanzibari ni rahisi kulazimishwa kukariri kuwa Zanzibar si nchi wala dola bali si rahisi kumfanya aamini hivyo. Kulazimisha uundaji wa vyama viitwavyo vya kitaifa baina Tanganyika na Zanzibari ni kitendo kisichokuwa cha kihalali, kisichokuwa na msingi na ni kitendo potofu. Hatua nyingi za kisiasa ni hatuwa za muda na za kupita, sio hatua za kimaumbile; ni hatua zinazotungwa na kupitishwa na binaadam na kila kina- choundwa na binaadam kinaweza kubadilishwa yaani si cha milele au cha kudra na lazima kama roho. Mwenye Enzi Mungu ndie anayeumba binaadam na kuwapa roho na maisha, kuwapa uume na uke, na kuwapa makabila na sura ili wajuane. Vile vile kuwapa viton- goji, vijiji, mashamba na miji, nchi na mataifa ili waishi pamoja, wajiongoze, kujitawala na kuheshimiana. Ikiwa mtu au watu watachukuwa wadhifa wa Mwenye Enzi Mungu, ata au watakuwa wanakosea na yale watakayo ya jaribu kuyabadilisha yatawashinda na hatimae kuwarudi. Nchi, kiini cha taifa, haiundwi kama ilivyokuwa watu hawaundwi bali huumbwa. Majaribio ya kutaka kuliumba taifa la Tanzania yamezidi kuwa katika sarakati ’lmawti (likikata roho) tokea Watanganyika walipozidi kuvinjari na kulidai taifa lao wenyewe na Bunge lao wenyewe. Khatua hii imedhihirisha zaidi kukuwepo kwa mataifa mawili huru, kinyume na madai ya hapo kabla kwamba Taifa lilikuwa ni moja tu. Sasa wimbo wa kuwasingizia Wazanzibari kutaka kujitenga umeanza kupunguwa kasi na ukweli wa mataifa mawili huru yaliyoungana, kuzidi kujichomoza. Zaidi ya yote hayo mara nyingi watu husahau kwamba Tanzania si nchi bali ni: "Jamhuri ya Muungano wa TanZania, "iliyoundwa kwa makubaliano ya watu wawili tu, Nyerere na Karume.