MISINGI YA VYAMA VYA KISIASA ZANZIBAR

Misingi ya vyama vya kisiasa Zanzibar

Ilikupata ufafanuzikamili, madhubutina wa kinaganaga kuhusu asili na misingi ya vyama vya kisiasa Zanzibar, hapana budi kutafuta msaada kutokana na historia ya Zanzibar kwa jumla na historia ya tawala zake makhsusan. Historia ya Zanzibar hasa ya kisiasa ina upungufu mkubwa, na inahitaji uchunguzi na uchambuzi wa makini wa kisayansi na ulio huru. Uchunguzi huu ni mgumu sana kwani mara nyingi utafiti wa historia unapambwa kupendeza utawala uliyopo kama utakuwa unaandikwa wakati utawala wenyewe ukiwa khatamuni, au kuambatana na aina ya siasa au idiologia ya muandishi au ya utawala unao- husika. Kuna watuwengi wananadhariaya kuweza kuandika au kushirikikatikauandikaji wa historia ya punde ya Zanzibar, lakini ama wamekuwa wakiogopa kutokana na utawala katili wa Zanzibar au utawala kandamizi wa Muungano, au kupungukwa na hamasa za kisiasa waliyokuwa nazo watu hao kiasi cha miaka 30 na 40 iliyopita. Kuna wengine wanachelea kuandika kwa sababu ya mazoefu mabaya ya usiri au kungojea mabadiliko ya serikali, mambo ambayo ama yanapotosha historia kutokana na upungufu wa kuweza kukumbuka au kutokana na vifo ama vya kawaida au vya kuuwawa kutokana na sababu za kisiasa. Vile vile usiri huo unasaidia serikali za kikandamizaji kuzidi kubaki katika utawala kwa vile wananchi wanakuwa hawaujuwi ukweli sahih uliyopitika nchini.

Ni matumaini ya kijitabu hichi kwamba, wale wenye ujuzi wa kihistoria muhimu wata- jitokeza na kuchangia kumbukumbu muhimu kama hii na kwa hivyo kuwafichuwa wale wanaoandika historia ya uwongo na ya kupendeza watawala. Ni jambo la maana kwa hivyo kudokeza kidogo juu ya mgawanyiko wa jamii ya Kizanzibari wa tokea enzi za kale ili kufahamu mfumo wa matabaka yaliyosababishwa na mgawanyiko wa jamii hizo. Hichi ni kijitabu kidogo ambacho hakiwezi kuieleza au kuifafanua historia ya Zanzibar ambayo ni nyingi na ya kupepea. Kijitabu hichi hakidai kutoelemea upande fulani wa kiidiologia, ingawaje kinajaribu kwa kadri inavyowezekana kuchambua hali halisi na ya kinaganaga ili kutoa mwangaza katika mambo fulani ambayo ingawa wengi wanayajuwa, lakini bado hawajaamuwa kuyaeleza.