MZIZI WA FITINA


Mzizi wa fitina
Mzizi wa fitina wa siasa ya Zanzibar uko katika historia, na kabla mzizi huu haujakatwa hapatokuwa namaendeleoya maanayakuwa nufaisha Wazanzibar ikwajumla. Zanzibarni nchi yenye historia ndefu na nyingi, hasa kufananisha na eneo lake, ilitajirika kutokana na maingiliano yake na kila aina ya watu wenye sifa mbali mbali bora na za kupigiwa mifano, watu waliyotoka sehemu mbali mbali ulimwenguni. Kuingiliana kwa Wazanzibari na staarabu mbali mbali tokea nyakati kabla kuzaliwa Nabii Issa I‘bn Mariam, kumeifanya Zanzibar iwesehemumojawa poyenyesifan jemanausta arabwa kuwekewamfano. Katika watu wa kale waliyotajika na waliyovuma kwa kiwango cha juu cha ustaarabu na elimu ilikuwani Machina, Wahindi, Wamisri na Wagirigi. Zanzibar ilifaidikakupata matunda ya staarabu hizo tokeaenzi za kale. Zanzibar ilitembelewana wataalamuna wafanyabiashara na wavuvi kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni, na baadhi yao walipendezwa na majira hayo na utu wa majira hayo na kuamuwa kugeuza Zanzibar makwao na kutotaka kurudi tena walikozaliwa, hapo wakaowa na kuzaliana na kuchanganya damu. Wengi wa hao walitoka sehemu za Arabuni, Uajemi, Barahindi, Uchina n.k. Wengi wao walikuwa ni wafanya biashara, wavuvi, mafundi, maagenti, wataalam na wana ahli l kitaab. Misafara hiyo na uhamiaji huo ulitokea zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita kabla ya utawala wa Mashirazi, Wareno, Waomani au Wangereza; ingawa kuja kwa watawala hao baadae nako kulichangia na kuhaibisha ustaarabu na utamaduni wa Zanzibar kwa kiwango fulani. Wahamiaji kutoka Arabuni, Barahindi na Shiraz walihamia Zanzibar kwa sababu tofauti. WahamiajiwaKishirazi wamwanzokatikaAfrikaya Masharikiwanasemekana waliwasili Afrika ya Mashariki katika karne ya sita (The Arab Chronicles of Kilwa). Wahamiaji ha wa walihama makwao ama kwa sababu za kisiasa, kidini au kibiashara. Katika karne ya 10 baada ya vita vya ukhalifa huko Uajemi, Sultan Hassan wa Shiraz pamoja na wanawe sita wa kiumena majahazi yao saba kwa jumla yalitweka kutoka Shirazi, hukoUajemi, leo kujilikanako kama Iran, yakaelekea Afrika ya Mashariki. Baada ya ku wasili pwani pwani mwa Afrika ya Mashariki Washirazi hawa wakaendeleza utawala wao wa kifalme katika Afrika ya Mashariki. Ishara na kumbukumbu zake bado ziko dhahiri pwani pwani mwa Afrika ya Mashariki yote. Ukumbusho madhubuti katika visiwa vya Unguja na Pemba ni ule wa Ufalme wa Mwinyi Mkuu, mfano mwema wa Mzanzibari aliyechanganya damu akiwa na asili ya Kishirazi na Kizanzibari. Karne tano zilipita kabla Wazungu kuishitukia Afrika ya Mashariki na Kati na mapambano makubwa ya mwanzo aliyoyapata Mwinyi MkuuyalikuwaalipopambananamkoloniwaKireno(RuyLourencoRavasco 1503)katika Unguja Ukuu, ambako kwa wakati huo ulikuwa ndio mji mkuu wa Zanzibar na baada ya kushindwa na kusalim amri Wazanzibari hao na Mfalme wao walilazimishwa kulipa kodi ya kila mwaka kwa mfalme wa Ureno. Katika mwaka 1509, mkoloni wa kireno, Duarte deLemos, aliwasili Zanzibar kudai ushuru au kodi hiyo kuto ka kwa Wazanzibari, ambao waligomakulipakodihiyo,nahapopakapigwavitadhidiyamajeshiyaKirenoyaliyokuwa na silaha bora zaidi za mabunduki na mizinga. Wazanzibari wakashindwa kwa mara ya pili, kukimbilia misituni, huku nyuma Wareno wakaendelea na kwiba, kunyang’anya, kuteketeza na kufisidi. Vita hivyo vilimfanya Mwinyi Mkuu akimbize watu wake na ufalme wake kutoka katika ufukwe wa bahari na kujifichia maporini na hatimae kujenga ngome yake huko Dunga.

Kwa mara ya mwanzo, Wareno walipowasili Afrika ya Mashariki walistaajabishwa sana na kiwango cha juu cha ustaarab. Kukuta mavazi ya haiba, ya lasi na haririr ya tunu na tamashana, ujenzi wa sifa na ustadi wa kifani, uliyopendeza na kupambika. Wakakuta ustaarabu uliyozalika kutokana na maingiliano ya karne na karne baina ya Afrika ya Mashariki na madola ya mashariki ya kati hadi mashariki ya mbali, kutoka Yemen hadi UchinanaJapan. Wareno,kablakufikaAfrikayaMashariki,walipitiaAfrikayaMagharibi, na walitarajia kuikuta Afrika ya Mashariki katika kiwango cha ustaarabu sawa na ule waliyoukuta Afrika ya Magharibi, lakini walistaajabishwa mno na kupigwa na mshangao kukuta majenzi na mavazi ya haiba na kupendeza kabisa, na Wanaafrika wa Mashariki walidharau kwa kejeli thamani ya zawadi walizoletewa na Wareno hao. Zanzibar kwa wakati wote kabla ya hapo, yaani kabla hata ya kuzaliwa kwa Nabii Issa, lilikuwa ni soko muhimu sana katika Afrika ya Mashariki na ya Kati, na kushughulika na biashara ya vipusa, ngozi, nyangumi, miti, nafaka, mbao n.k.