ZANZIBAR NI NCHI NA TAIFA HURU


Zanzibar ya kale
Kiasi cha miaka millioni mia moja na khamsini (150 million) iliyopita Barahindi ilikuwa ni sehemu ya Bara la Afrika na hatimae baada ya mgawanyiko wa pole pole wa ardhi, Barahindi ikaelea elea hadi kujiegeza na ile milima leo ijulikanayo kama Milima ya Hi- malaya. Ardhi na nafaka za Barahindi, miti na misitu yake, ufukwe wake wa pwani uliyojaa minazi, viungo vyake (pili pili, mabizari, karafuu, mdalaasini, hiliki, achari to- fauti n.k.), matunda yake (shoki shoki, madoriani, matufaa, embe), ndege wake, vinyama vyake (komba, manyani, makima na tumbili), wanyama wake (tembo na chui) vyote hivi vimefanana mno na hali ya Zanzibar, ingawa tembo na chui, kama vile nyangumi, kasa, kobe na mamba, wametoweka Zanzibar kutokana na usasi wa kibiashara wa vipusa. Mi- fano ya ardhi, wanyama na kadhalika kama hao wanaonekana sehemu mbali mbali za mashariki ya karibu na za mashariki ya mbali kama Sri Lanka, Singapore, Malaysia, Indonesia n.k.; wakati Malagasy, Ngazija na Mroni, Sheli-sheli (Seychalles), Sokotra n.k. zikiwa mashariki ya kando, zina mlingano kama huo na Zanzibar. Kuna baadhi ya wataalam wananakili kwamba visiwa viwili vya Unguja na Pemba vinatokana na asili tofauti, wataalamu hao inaonyesha wamesahau kwamba asili ya Barahindi inaambatana na ufukwe wa Mashariki ya Afrika, vile vile wataalam hao, na wale wanaowakariri, kwa sababu zao za kisiasa, wakijaribu kuuhalalisha Muungano, wanasahau tofauti ya ardhiya kusini Ungujayaani Makunduchi/Mtende/ Kibuteni/Kizimkazi,zikiwa naudongo mwekunduna mawe na majabali, ikifananishwana ardhiza Ungujaya kati na ya kaskazini zikiwanarutubatofauti. Kwamujibwahistoriaya kaleya enzizetu, kuambatananamaan- dishi ya "Perpulus of the Erythran Sea" na "Claudius Ptolemy", Edris, Chronicles of Kilwa n.k. Zanzibar (Menouthias Island) ikijulikana kama nchi iliyokuwa na biashara na nchi mbali mbali za Arabuni, Barahindi, Uchina na Japan tokea enzi za kale. Katika maandishi hayo ambayo ni katiya ya zamani kabisa kuhusu Afrika ya Mashariki hakujatajwa nchi au taifa lijulikanalo kama Tanganyika. Hadi April 28, katika mwaka wa 1885, sehemu ya Mrima ikijuli kana kama ni Mamlaka ya Bara ya Sultani wa Zanzibar. Tarehe hiyo yaani 28 April, mwaka 1885 ndiyo tarehe Serikali ya Kijarumani alipoamua kuzinyakuwa maili 60,000 za eneo la Mrima. Baada ya hapo ndipo makubaliano baina ya Mngereza na Mjarumani yakafikiwa, Muingereza ikachukuwa Hegoland, kama kiinuwa mgongo, na Mjerumani kuchukuwa Mrima. Unyakuwaji wa Wazungu wa ardhi ya Bara la Afrika, ulitokea baada ya Mfalme wa Belgium kuitisha mkutano wa nchi zilokuwa zikiongoza Ulaya katika mwaka 1876, huko Brussels, Ubelgiji. Muda mrefu sana kabla ya hapo Zanzibar ilikwisha julikana kama ni nchi, taifa na dola kamili, kinyume na Tanganyika.